Murkomen, mariga

Waheshimiwa Murkomen na Kamket warushiana cheche za matusi kuhusu Kibra

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amelumbana na  mbunge wa  Tiaty  William Kamket  ambaye alidai kwamba juhudi za naibu wa rais William Ruto kutawala eneo la Kibra zimefeli.

Hii ni kutokana na kushindwa kwa mgombea wa chama cha Jubilee McDonald Mariga ambaye anasemekana kuteuliwa na kupigiwa upato na naibu wa rais William Ruto.

Gavana Wa Mombasa, Hassan Joho Alazwa Hospitalini

Kamket alisema kwamba Ruto amefeli kupanda mbegu Kibra baada ya mgombeaji wa chama cha Jubilee McDonald Mariga kushindwa na Imran Okoth.

Akimkashifu Kamket, Murkomen ambaye pia ni kiongozi wa walio wengi katika Seneti alimtetea Ruto huku akimsifia kwa bidii zake.

Aidha, alimkemea Kamket kwamba umaarufu wake katika Baringo umedidimia.

Malumbano hayo yalitokea muda mfupi tu baada ya Ruto kupongeza Jubilee kwa kinyang’anyiro hicho cha Kibra.

Ruto alimpongeza McDonald Mariga na chama cha Jubilee kwa kuvamia na kudhibiti ngome ya Raila.

Ijumaa asubuhi, Imran Okoth wa ODM alitangazwa kuwa mbunge mteule wa eneobunge la Kibra.

Mariga Akubali Kubwagwa, Amualika Imran Chakula Cha Mchana – Video

 

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments