Wahubiri wa SDA walaumu maafisa wa polisi kwa wizi wa fungu la kumi

Waumini wa kanisa la SDA la Ranen waliandaa maombi halisi ya maafisa sita kutoka kituo cha polisi cha Awendo wanaokisiwa kuvamia kanisa hilo na kutoweka na sadaka na fungu la kumi.

Kulingana na mchungaji wa kanisa hilo, Jack Oyungu, maafisa tano wa kanisa hilo walikuwa wakifanya Kazi iliyohusisha kufanya hesabu za sadaka, kabla ya maafisa hao kuwavamia.

“There was no church service as instructed by government, the five were officials who were counting tithe and offering from members in basins when the officers came in,” Oyungu alisema.

Alisema kuwa fedha hizo zilikuwa zimeletwa na waumini kwa mda wa wiki hiyo.

Mchungaji huyo alisema kuwa watano hao walikuwa wamevalia mask kabla ya maafisa hao kuingia katika kanisa hilo.

“I was in my house which is in the church compound. When I heard the commotion, I went to check and the officer threatened to arrest me when I asked why they were harassing people inside the church,” Oyungu alisema.

Kulingana na Oyungu maafisa hao walitoweka na kiasi cha Sh35,000 fedha ambazo zilikuwa zimehesabiwa, na fedha zingine ambazo hazikuwa zimehesabiwa ambazo zilikuwa ni fungu la kumi.

“They pretended to have arrested the five people, walked with them about 300 meters from the compound and released them before returning the money and taking off with about Sh6,000,” Oyungu alisema.

Akizungumza kupitia simu, OCPD wa Awendo Mary Musyoka alisema maafisa wa kanisa hilo bado hawajapeana taarifa yoyote kwa polisi ili utafiti ufanywe.

“We need them to give an official complaint for investigations to commence, so far we only heard their complaints through the media,” alisema.