Wahudumu wa boda boda wakamatwa katika msako wa kukabili uhalifu

Ni kwa muda sasa wakaazi wa mitaa Milimani na Kileleshwa wamekuwa wakiishi kwa hofu kwa sababu ya kutishiwa maisha na wahalifu katika eneo hilo.

Jana washukiwa wanne  wa walikamatwa na polisi katika eneo hilo.

Abdul Jafar, Derick Simani, Sadiq Mohamed na Hassan Musa Kipkoech walikamatwa jumapili jioni na sasa wako mikononi mwa polisi.

"Kufuatia  kuongezeka kwa  visa vya ahalifu wanaojifanya wahudumu wa bodaboda, katika mitaa ya Kilimani na Kileleshwa  operesheni inaendelea na watuhumiwa wanne wametiwa mbaroni kwa sasa," DCI Alisema.

Bastola moja na pikipiki mbili ambazo hazikuwa zimesajiliwa zilipatikana.

Wanne hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao.

Mwaka jana Mkurugenzi wa idara ya jinai aliwakamata washukiwa wa uhalifu ambao walikuwa wanawahangaisha wakaazi wa eneo la Kileleshwa.

Walikamatwa baada ya DCI kutazama kamera za CCTV na kuwawekea mtego.

Gari jeusi aina ya Prado pia liliweza kuonekana katika kamera za CCTV na linazuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

DCI aliandika katika mtandao wake wa kijamii kuwa washukiwa wanazuiliwa na polisi.

DCI KENYA

@DCI_Kenya

Following reports of increased cases of criminals operating on Boda bodas within Kilimani & Kileleshwa, detectives based at Kilimani mounted an intelligence led operation where four suspects namely Abdul Jafar, Derick Simani, Sadiq Mohamed..

DCI KENYA@DCI_Kenya

.. and Hassan Musa Chepkoech were arrested.

One pistol, motor cycles registration number KMFA 500Z, KMET 389K and two other numberless ones were recovered and detained.

Je watuhumiwa hao wataachiliwa huru ama mahakama itachukua hatua ipi ili kuwezesha wamejibu mashtaka yao inavyostahili na ni hukumu gani ambayo watapewa baada ya kupatikana na hatia?