Wahudumu wa bodaboda watishia kuteketeza magari aina ya probox, Busia

Wahudumu wa bodaboda mjini Busia wametishia kufanya maandamano na kuteketeza magari aina ya probox ambayo huwagonga na kuwauwa wahudumu wa bodaboda kila siku kwenye barabara ya mjini huo.

Mwenyekiti wa wahudumu hao kaunti ya Busia, Eric Makokha amesema inasikitisha kuona wahudumu wa bodaboda wakiuwawa kila uchao na magari hayo ambayo husafirisha bidhaa za magendo kwa mwendo wa kasi.

Kisa cha hivi punde ni cha jana usiku ambapo muhudumu mmoja wa bodaboda ya baiskeli aligongwa na moja wapo ya magari hayo na kufariki papo hapo katika eneo la Sherman huku gari hilo likitoweka.

-Leonard Ojiambo