waiguru-compressed

Waiguru ampongeza Imran, asema ni ‘zao la Handshake’

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amempongeza mbunge mteule wa Kibra Bernard Imran Okoth kwa ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanywa Alhamisi.

Kupitia mtandao wake Twitter, Waiguru alimpongeza Imran Okoth huku akisema ni “Zao la Handshake’ katika uchaguzi huo mdogo.

Makosa Aliyofanya MacDonald Mariga, Angembwaga Imran Okoth

Waiguru ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wa Jubilee waliojitokeza hadharani kumpigia kampeni Imran Okoth wa ODM licha kwamba kulikuwa na mgombeaji McDonald Mariga wa chama chake.

PATANISHO: Baba Alibomoa Nyumba Yangu Na Kupeleka Mabati Kwa Chifu

Gavana wa zamani wa Kiambu pia alimpongeza ushindi wa Imran.

IEBC imemtangaza rasmi Imran Okoth wa ODM kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Kibra. Okoth alipata kura elfu 24,636, akifuatiwa na mwaniaji wa Jubilee McDonald Mariga aliyepata kura 11,230.

Eliud Owalo wa ANC alipata kura elfu 5,275.

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments