Hatimaye Waiguru na Waiganjo wafunga pingu za maisha(Picha)

Harusi ya gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru imefanyika leo. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na watu mashuhuri kama vile, Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, Dennis Itumbi na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Murang'a Sabina Chege.

Waiguru aliingia kwenye sherehe aliwasili kwenye sherehe huku akikaribishwa kwa nyimbo na densi za kitamaduni.

Baada ya mbwembwe na sherehe na densi Waiguru na mumewe Waiganjo walidhihirisha kuungana kwao kama mke na mume kwa kukata kiande, inayomaanisha kukata kipande cha bega ya mbuzi aliyechomwa. Kwa jamii ya wakikuyu hii ni ishara kuwa wawili hao wamefunga pingu za maisha.

Katika sherehe hiyo bwana harusi hukata upande wa kulia wa mkono wa mbuzi aliyechomwa huku bi harusi akiwa ameshikilia upande huu mwingine. Anapomaliza, anamlisha mke wake alfu kisha anakula yeye kuashiria kuwa atailinda familia yake.