Wairimu alimnyima Cohen haki kitandani kwa miaka 4

Tendo la ndoa, dhulma na mali ni maswala yaliochangia talaka baina ya Mholanzi Tob Cohen na mkewe Sarah Wairimu, kulingana na stakabadhi za kesi zilizofikia gazeti la The Star.

Stakabadhi za kesi hiyo zilizofikia gazeti la The Star zaonyesha picha ya ndoa iliojaa uhasama, uhasama uliokuwa umefika kiwango cha kutorekebika na hata hapakuwepo tendo la ndoa.

Mfanyibiashara huyo mholanzi alionekana kufanya kila juhudi kumuondoa Wairimu kutoka boma lao la Lower Kabete, kulingana na stakabadhi hizo.

S

Cohen aliripotiwa kutoweka mwezi Julai na polisi wakaupata mwili wake katika tangi la chini ya ardhi nyumbani kwake Septemba tarehe 13. Alikuwa ameuawa kinyama. Mjane wake Wairimu, mwenye umri wa miaka 52 anazuiliwa katika Gereza la wanawake la Lang’ata na anatarajiwa kula kiapo kuhusiana na mauaji hayo siku ya Jumanne wiki hii.

Ni Cohen mwenye umri wa miaka 71 alikuwa wa kwanza kuwasilisha kesi ya kutaka talaka tarehe 21 mwezi Januari chini ya cheti cha dharura. Alidai kwamba Wairimu alimnyima ngono tangu mwaka 2014. Alisema walikuwa wakilala katika vyumba tofauti na kwamba alikuwa akijitayarishia chakula chake.

Februari 25, Cohen alifanyia marekebisho sababu za kutaka talaka na kuongeza dhulma na fujo zilizokuwa zikitekelezwa na Wairimu. Mfanyibiashara huyo alisema kuna siku Wairimu aliingia ofisini mwake kwa fujo na kumwagia maji na kumwonya, "Usidhani kuwa haya yameisha, hiajaisha."

Pia alisema kwamba siku nne baadaye, Wairimu alimshambulia, na kumweka majeraha kadhaa… hii ilimsababishia machungu na masumbuko mengi. "[Baada ya kumsukuma kutoka ngazi ya ghorofa ndani ya nyumba yao]..akiwa amelala chini, akitokwa damu, Wairimu alimkalia na kuanza kumpachika mangumi na mateke," Wakili Judy Thongori alisema katika mawasilisho yake.

Cohen alitaka OCS wa kituo cha polisi cha Spring Valley, kumfurusha Wairimu kutoka boma lake huku wakisubihri kesi ya talaka kuamuliwa. Mwaka 2015, ndoa yao ilipoanza kuzorota, Wairimu aliwekea shamba lao kikwazo ili kuzuia jaribio lolote la kuuza shamba hilo, kulingana na stakabadhi zilizopatikana na gazeti la The Star. Stakabahdhi hizo zaonyesha kuwa Cohen alijaribu kuondoa kikwazo hicho kupitia ombi la Julai 1, 2019.

Majibu ya Wairimu

Lakini katika majibu yake chini ya kiapo, Wairimu “anakiri ndoa yao ilikuwa na matatatizo yasioweza kusuluhishwa lakini anadai kuwa sababu kuu ni kutokana na usinzi na ukatili kwa upande wa Cohen]."

Anakariri kwamba pia alitaka talaka, Wairimua alipuuzilia mbali madai kwamba alikuwa mtu wa fujo, akihoji kuwa ilikuwa njama ya Cohen kuonyesha picha ya mke katili.

Mashambulizi yalinzishwa na Cohen aliyepanga matukio hayo ili kupata sababu katika ombi lake la kutaka talaka.

Pia alipuuzilia mbali madai ya kumnyima Cohen haki zake za unyumba, akisema kwamba walilala pamoja katika chumba kikuu isipokuwa siku ambazo walikuwa wamekosana “ alipolazimika kulala katika chumba cha bintiye [Renee] Gathoni wakati Cohen alikuwa akitumia vileo na kumdhulumu."