Waislamu washerehekea Idd-Ul Adha licha ya janga la corona

Waislamu kote nchini wameanza kusherehekea Idd Ul Adha   baada ya kutamatika kwa  Hajj.

Kila mwaka  waislamu husherehekea Idd Hiyo ya kuchinja  mfugo pamoja na  familia ,marafiki na jamii baada ya salah ya  alfajiri  na kisha baadaye kuwagawa watu chakula  na misada mingine kwa wanaoihitaji .

Hata hivyo mwaka huu kwa ajili ya janga la corona wengi wamelazimika kubadilisha jinsi wanavyosherhekea Idd kwani serikali hairuhusu wtau wengi kungomana katika sehemu moja.Salah ya Idd  katika maeneo mengi imefanyika kwenye viwanja na maeneo ya wazi

Idd-ul-Adhais  huadhimishwa kila siku ya 10 ya mwezi wa  Dhul Hijja ,wa mwisho katika kalenda ya mwezi wa kiislamu  kwa salaha ya asubuhi ,kuchinja mfugo  -hasa kondoo  kama kumbukumbu  wakati nabii Ibrahim  na mwanawe  Ismael .

Rais Uhuru Kenyatta  na viongozi mbali mbali alhamisi walituma jumbe za kuwatakia waislamu Idd njema .