Wajir ni miongoni mwa kaunti 10 fisadi zaidi kulingana na EACC, 2019

EACC-compressed
EACC-compressed
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imeorodhesha kaunti zinazoongoza kwa ufisadi chini Kenya.

Ripoti ya uchunguzi iliyofanywa mwaka uliopita inaorodhesha Tana River kuwa kaunti fisadi zaidi na asilimia 3.76 huku ikifuatwa na Kilifi kwa asilimia 2.17.

Wananchi katika maeneo hayo fisadi zaidi wanasemakana kutoa hongo ili kupata huduma za kiserikali.

Kaunti ya Lamu na Wajir inashikilia nafasi ya tatu huku takwimu zikionyesha kuwa asilimia 1.9 ya watu hutoa hongo.

Aidha, Kisii, Vihiga, Garissa, Laikipia na Mandera ,West pokot inaongoza kwa ufisadi katika taasisi pamoja na watu wanaotoa hongo ili kupata huduma.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa kiasi cha shilingi 14,354 hutolewa kama hongo katika eneo la Wajir, ikifuatwa na Kitui kwa shilingi 11,640, Kericho 11,265.

Hata hivyo Samburu, Nyamira, Kisumu, Embu, Homabay, Baringo na Isiolo ni kaunti yenye idadi ndogo ya kesi za ufisadi.

Kulingana na EACC kiwango cha wastani cha hongo mwaka 2018 ni 3,833 ikilinganishwa na 5,000 mwaka wa uliotangulia.