Katika ulingo wa soka, Messi yupo kileleni kwa wale wanaotiia kikapuni mpunga mkubwa sana ambayo ni maradufu zaidi ya kile mshindani wake Ronaldo anapata kila mwezi.
Kulingana na ripoti iliyochapishwa na L’Equipe, nyota wa Barcelona Lionel Messi anaongoza kutokana na kiasi kukubwa cha mshahara anayolipwa.
Mwajentina huyu ambaye hucheza kama kiungo wa mbele , hutia mfukoni kima cha pauni milioni 8.3, hii ni takribani shilingi milioni 957,874,833.95 kila mwezi.
Naye nyota wa Ureno, ambaye aligura Real madrid na kujiunga na Juventus analipwa kima cha pauni milioni 4.7 kila mwezi ambayo ni shilingi milioni 542,445,183.36.
Ronaldo ndiye mwanasoka wa pekee anayecheza kule Italiano ambaye amerodhoshwa kwenye 10 bora.
Hata hivyo, Hispania inaongoza katika orodha hiyo wakiongoza huku watano kati yao wakichezea ligi ya La Liga.
Hii hapa ni orodha ya wachezaji 10 wa soka wanaolipwa donge nono kila mwezi kabla ya kutozwa ushuru:
1. Lionel Messi (€8.3 Million)
2. Cristiano Ronaldo (€4.7 Million)
3. Antoine Griezmann (€3.3 Million)
4. Neymar (€3.06 Million)
5. Luis Suarez (€2.9 Million)
6. Gareth Bale (€2.5 Million)
7. Philippe Coutinho (€2.3 Million)
8. Alexis Sanchez (€2.28 Million)
9. Kylian Mbappe (€1.73 Million)
10. Mesut Ozil (€1.6 Million).