Wakaazi wa Hola wafunga barabara wakiitaka serikali kuwapa makaazi mapya

EYSO6vNX0AAMkhn
EYSO6vNX0AAMkhn
Kutokana na mvua nyingi inayoendelea kunyesha nchini na kusababisha vifo na watu kukosa makao, wakaazi wa Hola kutoka kuanti ya Tana River wameifunga barabara hii leo ili kushinikiza serikali ya kaunti hiyo kuwapa makaazi mengine baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.

Kaunti ya Tana River ni miongoni mwa kaunti nchini ambazo zimeathirika pakubwa kutokana na mvua inayoshuhudiwa nchini huku watu zaidi ya 6,000 wakisema kuwa wamekosa mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.

Inadaiwa kuwa bahari Hindi limejaa zaidi hali ambayo imewalazimu wakaazi wanaoishi karibu kuhama makwao ili kuokoa maisha yao.

Kufikia sasa, yamkini wakenya zaidi ya 237 wamefariki kutokana na mafuriko hali ambayo inaipa serikali kiwewe .