Wakati umefika!Jacque Maribe aonyesha sura ya baba ya mtoto wake

Je unajua kuwa Jacque Maribe ana mtoto?
Kidosho huyu aliyekuwa mtangazaji wa televisheni ya Citizen ana mtoto mmoja wa kiume na hakuna siku ambayo amewahi kuonyesha sura ya baba ya mtoto wake.

 

Hata hivyo Jacque Maribe alihudhuria sherehe ya kuhitimu kwa mtoto wake wa kiume shuleni na pamoja naye alikuwa baba ya mtoto wake.

Amini usimini, babake mtoto huyu  Zahari ni mcheshi Eric Omondi.
Wawili hawa wamekuwa marafiki kwa muda mrefu na wao hulea mtoto wao Zahara pamoja.

Baada ya sherehe hiyo, kupitia mtandao wa Instagram, Jacque Maribe aliweka picha akiwa na baba ya mtoto wake na kuandika,
"Family first. Happy graduation day Zahari. We, mum and dad @ericomondi are proud of you."

https://www.instagram.com/p/B3uLGIlnV9r/