Wakazi wa Bungoma waishi kwa hofu baada ya kuvamiwa na chui

fisi
fisi
Wakaazi wa kijiji cha Nalondo eneo bunge la Kabuchai huko Bungoma wamelalama kuvamiwa na mnyama mmoja ambaye hajulikani na amekuwa akiwaua mifugo wao na kutishia kuwauma wakaazi mida za usiku.

Wakiongea na wanahabari wakaazi hao ambao wanaishi kwa hofu wakiongozwa na Benjamin Mauko ambaye amewapoteza ngombe wake wawili wametaka maafisa kutoka shirika la KWS kuingilia kati na kunasa mnyama huyo kabla haja sababisha maafa zaidi.

Mauko aidha amehofia kwamba huenda wakaazi wanauziwa nyama ambao wamefariki baada ya kuumwa na myanma huo ambaye kwa sasa amewaua zaidi ya mifugo ishirini wakiwemo ngombe, mbwa kondoo na hata mbuzi.

Tukisalia Bungoma, wakaazi wa kaunti hiyo wametakiwa kujitokeza kwa  wingi ili kushiriki vikamilifu kwenye zoezi la kuhesabiwa kwa watu  kote nchini, almaarufu kama census.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na maafisa wa usajili wapatao 603  kaunti kamishina wa Bungoma Stephen Kihara  amesema kuwa vikosi vya usalama viko tayari kutoa ulinzi wa kutosha wakati wa zoezi hilo.