Wakazi wa Shinyalu washangazwa baada ya ng'ombe wao kukatakatwa

Wakazi wa kijiji cha mnasio wadi ya isukha magharibi eneo bunge la shinyalu kaunti ya Kakamega wameshangazwa na kitendo cha watu wasiojulikana kukatakata ng'ombe wa maziwa wa mjane mmoja eneo hilo.

Mjane huyo Letisha Mulamula amesema anaishi kwa hofu baada ya kufanyiwa uovu huo mara kadhaa.

Mjane huyo alipohojiwa alikiri kuwa anaishi na woga tele kwani sio mara ya kwanza kushuhudia tukio kama hilo.

"Mfanyikazi wangu ndiye aliyeenda kukamua ng'ombe wa kwanza, alipoenda kwa wa pili ndio akaja akaniita. Nilipoenda kuangalia nikapata ng'ombe imekatakatwa, ng'ombe haisimami imelala tu chini huku miguu yote ya nyuma ikiwa imekatwa." Alisema.

Hayo yakijiri, zaidi ya asilimia 90 ya walimu waliostaafu katika kaunti ya Taita Taveta hawajapata malipo yao ya uzeeni licha ya kustaafu zaidi yamiaka sita iliyopita.

Katibu wa chama cha KNUT tawi hilo Lenox Mshilla ameilaumu serikali kwa kutoachilia fedha za wafanyikazi wa umma punde tu wanapostaafu akisema kuwa wengiwanaishi katika umasikini.

Ameitaka tume ya TSC kuharakisha ulipaji wa pesa hizo.