Wakenya 133 wamepatikana na virusi vya corona- Mutahi

3XPhNwR1.jfif
3XPhNwR1.jfif
Akihutubia taifa kutoka katika kunti ya Nyandarua hii leo, waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema wakenya wengine 133 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha watu 3727

Wakati uo huo Mutahi amesema watu wengine 33 wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 1286.

Mtu mmoja amefariki na kufikisha watu 104 waliofariki kutokana na virusi hivyo.

Mutahi amehimiza viongozi na washikadau wa kaunti ya Nyandarua kushirikiana kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeingia eneo.

Nyandarua ni miongoni mwa kaunti 9 nchini ambazo hazijasajili kisa chochote cha corona.

Amewataka wakenya kuzingatia masharti ya serikali kama njia ya kupunguza maambukizi.

Kwa upande wake gavana wa Nyandarua Francis Kimemia amesema jimbo hilo limetenga vitanda vya wagonjwa mahututi ICU 13 na ambavyo vilinunuliwa kwa shilingi milioni 70.

Ameongezea kuwa wametenga vitanda vingine 300 vya kuwatenga wagonjwa.

Kimemia vile vile amesema kuwa wamepokea vifaa vya PPEs 1,000 na watapeleka maeneo ambayo huenda kutaripotiwa virusi hivyo.