Wakenya 237 waliorejeshwa nchini kujitenga kwa siku 14 -Dr Rashid Aman

NA NICKSON TOSI

Akitoa taarifa yake ya kila siku kwa taifa kuhusiana na janga la Corona ,Katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman alisema kuwa wakenya 237 walioondolewa India na kurejeshwa nchini watalazimika kujitenga kwa siku 14 kama serikali ilivyowaagiza.

“I’m glad to inform you that 237 Kenyans, together with their family members and caregivers, arrived last evening and were received by staff from the Ministry of Health who facilitated their clearance,” alisema Aman.

Ndege ya shirika la Kenya Airways iliwabeba wakenya hao 237 waliokuwa katika taifa la India haswa kwa miji yua Mumbai na Shangai na walitia guu katika anga tua ya JKIA Alhamisi Usiku.

Kulingana na katibu katika wizara ya maswala ya kigeni Ababu Namwambu wengi wa wakenya hao waliorejea nchini walikuwa wameenda kutafuta tiba na jamaa zao kabla ya janga la corona kutokea.