Wakenya 2,500 hawawezi kuoa/kuolewa kutokana na corona

MARRIAGE
MARRIAGE
Kufunga ndoa wakati huu ambapo visa vingi vya corona vimekuwa vikiripotiwa nchini huenda ikawa vigumu, hali itakayokufanya usubiri hadi pale afisi ya msajili wa ndoa nchini itakaporuhusiwa kuanza kufanya shughuli hiyo na wizara ya afya.

Ofisi ya mkuu wa sheria nchini AG, Imesema inapania kufungua na kutumikia msongamano wa hafla za kufunga fungate za maisha ambazo zimejaa katika afisi hiyo baada ya kusitishwa ghaflaa.

“For now we are dealing with backlog. We are hoping that by Monday next week the Ministry of Health will come and inspect these premises and give us the go-ahead. Once the go-ahead is given, we shall start with the backlog,” amesema Winnie Guchu.

Kulingana na data kutoka kwa afisi ya msajili wa ndoa nchini, watu 815 walikuwa wametuma maombi ya kufunga ndoa kabla ya kutokea kwa virusi hivyo huku watu wengine 1,754 walikuwa wameanza mchakato wa kutuma maombi ya kuruhusiwa kufunga ndoa aidha kwa kanisa ama maeneo mengine.

“Only 22 marriages have not expired, the remaining 793 the 90-day period has expired and those couples will have to reapply so that they go go back to the 90-day period. If we do conduct those marriages outside the 90-day period those marriages will not be valid,” alisema Guchu.

 Changamoto kuu sasa kwa afisi ya msajili wa vyama nchini ni kubaini njia mwafaka ya kuweza kuzishughulikia barua za wakenya 2,500 waliokuwa wametuma barua za kufunga ndoa.

Taarifa kutoka State Law inasema kuwa inapania kuwaruhusu watu kuanza kutuma maombi ya kupata cheti cha kufunga pingu za maisha kupitia mitandaoni.

“We have digitised all the marriages processes and the Kenyan citizen will be able to make applications and payment for service electronically,” alisema Silas Oswe.