Wakenya tegeni maskio! Vitu ambavyo hupaswi kufanya unapopewa lifti

lifti
lifti
Msimu wa Krisimasi uko hapa na kama kawaida mipango ya usafiri kuelekea mashambani (ocha) ili kusherehekea na jamii walioko nyumbani.

Mara nyingi wengi husafiri kwa gari za umma ila kunao ambao hutumia gari za kibinafsi na hapo ndipo wengi hubahatika kupewa lifti.

Hata hivyo, wakenya wengi haswa kutoka Nairobi wanajulikana kwa tabia zao za kuudhi wanapopewa lifti na leo tunachambua tabia hizo huku tukiwapa mawaidha, jinsi ya kuwa na nidhamu.

1. Tafadhali jifunze kufika mapema kama mlivyo agana na mwenye gari

2. Usiweke mikono yako dirishani kama mdosi ili uonekane na watu

3. Kama anaye kupa lifti anasafiri na familia yake, tafadhali keti nyuma usije ukajiabisha ukipiganie kiti cha mbele na mkewe mwenye gari

4. Usisahau ukaanza kubadilika na kuwa DJ. Kama anaskiza Mayieng/Sulwe/ Chamgei FM usijifanye kimbelembele uweke Radio Jambo

5. Uliza kwanza kabla ya kufungua dirisha kwani kuna uwezekano huwa imeharibika

6. Ukigundua mwenye gari anasafiri na mwanadada mwingine ambaye sio mkewe, usianze kuuliza maswali za kijinga kwani waweza muaibisha

7. Jaribu sana kukosa kuuliza maswali za kiujinga kwa mfano "Gari kama hili ulinunua pesa ngapi"

8. Usigeuze gari la wenyewe kuwa lako la kubebea mizigo yako kutoka mashambani kwa mfano; Makaa, viazi, ndizi ukiwa safarini. Kwani ulikomboa lile gari?

9. Kumbuka sio gari zote hupitia Kencom au Ambassadeur kwa hivyo wapaswa kuwa tayari kushukia gari eneo lolote lile mjini Nairobi

10. Beba vitu vinavyofaa. Usianze kubeba kuku mzima, bata, mbwa au pia chang'aa kwani utachafua gari la wenyewe

11. La muhimu ni kuwa kabla ya kutumia gari la wenyewe lazima uoge na usiwe umekula vyakula vya kila namna na kuwaharibia wengine hewa ndani mwa gari

12. Usiwe mtu mkono gamu kwani itafika wakati na utatakiwa kuchangia fedha kwa mfano wakti wa kununua maji, chakula cha mchana au pia matunda njiani.