RAMAPHOSA

Wakenya waathirika na mashambulizi dhidi ya wageni, Afrika Kusini

Ubalozi wa Kenya nchini Afrika Kusini umethibitisha kuwa wakenya kadhaa wameathiriwa na mashambulizi yanayolenga raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

Wavamizi Afrika Kusini AFP
Katika taarifa, balozi wa Kenya nchini Afrika Kusini Jean Kamau alisema kwamba tayari wamewasiliana na jamaa walioathirika.

 

Mashambulizi dhidi ya wageni Afrika Kusini, Nigeria yachukuwa hatua

“Ubalozi wa Kenya umetamaushwa kwamba wakenya kadhaa wameathiriwa na mashambulizi wa hivi karibuni nchini humo kwa kupigwa na mali zao kuteketezwa moto katika maeneo ya mkoa wa Gauteng” alisema
“Tumewashauri kuzingatia maagizo na wito wa polisi wa Afrika Kusini kuripoti na kuandikisha taarifa kuhusu visa vya mashambulizi dhidi yao.”

 
Aliwatahadharisha wakenya kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wao ili kutathmini hali na kuchukuwa hatua za kujikinga.

RAMAPHOSA
“Wote wanafaa kuwa makini na kujifahamisha kuhusu mandharai wanamoishi,” balozi huyo aliongeza.
Wakati huo huo ubalozi wa Kenya unafanya mashauriano na maafisa wa serikali ya Afrika Kusini na wamehakikishiwa kwamba serikali ilikuwa inaweka mikakati kuimarisha usalama wa watu na mali zao.

 

Aliyemnyofoa sehemu za siri mmewe ashtakiwa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Jumanne alikashifu vikali visa vya mashambulizi na kuibwa kwa mali vikilenga raia wa nchi za kigeni.

 
“Hakuna sababu yoyote ile kwa raia yeyote wa Afrika Kusini kushambulia au kuwadhulumu rai wa nchi zingine,” alisema.

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments