Floods-compressed

Wakenya watahadharishwa, huku mvua kubwa ikiendelea hadi Ijumaa

Mvua kubwa inayoshuhudiwa kote nchini inatarajiwa kuendelea hadi wikendi.

Idara ya utabiri wa hali ya anga imeonya kuwa hali unyevu unyevu itatawala katika jiji la Nairobi, maeneo ya kati na kusini itaendelea kwa muda zaidi.

Hata hivyo, tahadhari imetolewa kwa wananchi kuwa mvua kubwa itashuhudiwa kuanzia Jumatano hadi Ijumaa na kisha kupungua ifikapo wikendi.

Utabiri wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mvua itaendelea kwa takriban kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Sarakasi: Jinsi Mgonjwa Alivyotoroka Kutoka Hospitali Baada Ya Upasuaji

Maeneo yanayotarajiwa kupokea viwango vya juu vya mvua ni  Nairobi, Embu, Meru, Nyeri, Kericho, Narok, Kajiado na Nakuru.

Maeneo mengine yanayotarajiwa kupokea mvua kubwa ni pamoja na Elgeyo Marakwet, Kakamega, Uasin Gishu, Machakos, Makueni, Kitui, Nyandarua, Laikipia, Murang’a, Taita Taveta, Kisii, Homa Bay, Kisumu, Siaya, Baringo, West Pokot na Busia.

Wakaazi wameshauriwa kuwa wangalifu mafuriko yanapotokea.

Tahadhari pia imetolewa kwa wale wanaoishi maeneo ya milima kuwa waangalifu dhidi ya maporomoko ya ardhi.

Msemaji wa serikali Cyrus Oguna Jumanne alisema kuwa zaidi ya watu 132 yamefariki kutokana na mvua iliokuwa ikinyesha.

Huku zaidi ya watu 17,000 wakiachwa bila makao.

Hivi Karibuni Dawa Za Kuzuia Ujauzito Zitauzwa Dukani Kama Kondomu

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments