Wakulima kutoka Taita Taveta wazusha kuhusu uvamizi wa ndovu mashambani yao

Elephants
Elephants
Mamia ya wakulima kutoka Sagala kaunti ya Taita Taveta hatimaye wameandikisha taarifa katika kituo Cha polisi Cha Voi kuhusu hasara wanayopata kufuatia uvamizi wa ndovu.

Wakulima hao ambao wanakadiria hasara kubwa sasa wanaitaka serikali kuwafidia mimea na mali yao iliyoharibiwa na ndovu ambao wamevamia maeneo ya Sagalla, Kirumbi na Kasighau tangu mwezi jana.

Kwingineko, vijana katika kaunti ya Taita Taveta watanufaika na masomo ya kibiashara pamoja na ufadhili wa kifedha kutoka kwa hazina ya maendeleo kwa vijana.(Youth Enterprise Development Fund) kupitia kwa mpango wa Youth Plus Mashinani.

Moris Murimi kutoka hazina hiyo anasema mpango huo utakaofanyiwa majaribio katika kaunti tatu unalenga kuwawezesha vijana kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu ubunifu wa biashara kupitia kwa kozi fupi za miezi sita.

Kwingineko, familia moja kutoka mjini Nambale kaunti ya Busia inaishi kwa hofu baada ya jamaa wao kutoweka nyumbani kwa njia isioeleweka.

Ziporah Wafula anasema mwanawe Daniel Abakar mwenye umri wa miaka 24 alitoka nyumbani tarehe 26/12/2018 na hadi leo hajawahi kuonekana huku juhudi zao za kumtafuta katika vituo vya polisi, hospitalini na hata kwenye vyumba vya wafu zikikosa kuzaa matunda.