Walimu wakuu wataka mitihani ya kitaifa kuahirishwa

Walimu wakuu wanataka mitihani ya kitaifa kuahirishwa wakisema kwamba ongezeko la maambukizi  ya coronavirus  huenda  likacxhelwesha kufunguliwa kwa shule.

Serikali ilizifunga shule zote mwezi machi  kwa sababu ya janga la coronavirus  na  tathminmi ya wizara ya afya kwamba huenda virusi hivyo vikafika kilele chake mwezi agosti inamaanisha kwamba muhula wote utakuw umekwisha bila wanafunzi kurejea shuleni .

“ Mitihani ya kitaifa inafaa kuahirishwa hadi wakati watahiniwa watakapokuwa tayari kuifanya .wiki kadhaa za masomo imepotea kwa sababu  shule zilifungwa ghafla  ,itakuwa muhimu baada ya shule kufunguliwa mikakati ifaayo iwekwe ili kuwapa wanafunzi maagizo ya kuweza kujifunza yote waliokosa’ muungano wa walimu wakuu umesema

Kalenda ya baraza la mtihani nchini KNEC inaonyesha kwamba mtihani wa KCPE   utaanza oktoba tarehe 27 ilhali ule wa KCSE  utaanza Novemba tarehe 2.

Rais Uhuru Kenyatta na waziri wa Elimu George Magoha wamesema kwamba kalenda ya mtihani  kwa watahiniwa wote milioni 1.8  itasalia jinsi ilivyopangwa .