‘Walitoroka na pesa za harusi , coronavirus ilipofika’

Virusi   vya corona  vimesababisha  visanga mbali mbali nchini lakini hakuna kinachowakwaza moto Peter na Jan ambao walifaa kufanya harusi yao  tarehe  tatu mwezi Aprili .

Kama wakenya wengi ambao huunda makundi ya whatsapp ili kuchangisha fedha za kufanikisha harusi yao , wao pia waliunda kundi kubwa la whatsapp ambalo lilikuwa na watu wa kanisa lao ,familia ,rafiki zao na watu waliokuwa wakifanya kazi nao.Mchango ulianza kutolewa mwezi januari na kufikia  mwezi machi walikuwa tayari wamepewa shilingi lakini nane ambazo zilikuwa  zikikabidjhiwa kamati maalum ua kusimamia maandalizi ya harusi yao.

Kamati hiyo ilikuwa na  mwenyekiti,mweka hazina ,karani na watu wengine wane . Pesa zliendelea kutolewa na walikuwa wamesalia na upungufu wa shilingi laki mbili ili kufikia kiwango walichotaka cha bajeti ya shilingi milioni moja ili kuandaa harusi nzito ya kutetemesha mtaa wao ,Ongata Rongai. Mambo yalianza kuwandemea vibaya tarehe  18 mwezi machi  wakati serikali ilipotangaza kupiga marufuku mikutano ya hadhara.Ilianza kubainika wazi kwamba huenda harusi yao haitafanyika kwani harusi nyingi zilianza kuahirishwa .

Wakati wote huo Peter na Jane walianza kujiuliza   kuhusu hatua watakazochukua endapo harusi yao haitafanyika siku waliyopanga kuifanya . Siku chache baadaye ,mwenyekiti  wa kamati ya kuandaa harusi alitangaza kwamba wamefutilia mbali mikutano yao ya kila mara ya kujadili matayarisho ya harusi  yao. Baadaye  ilianza kuwa vigumu kumpata kwenye simu .Walijaribu kuwasiliana na mweka hazina ambaye jukumu lake lilikuwa kuweka zile pesa ambazo walikuwa wamechangisha hadi kufikia wakati ule .Hawakumpata kwenye simu . hapo ndipo Peter na Jane walipoanza kushuku kuna tatizo lakini hawakufahamu shoka litakalowapiga litatokea wapi .

Tarehe 22 ,walipoamuka asubuhi walifaa kukutana na kamati ya kuandaa harusi ili wakabidhiwe pesa hizo waliziweke na zilizo kwenye mpesa zitolewe ili wajue watakavypozihifadhi wenyewe hadi tarehe mpya ya harusi itakapotangazwa . walipofika katika eneo walilofaa kukutana hawakumuona yeyote kati ya wanachama wa ile kamati .Walipoingia mtandaoni kwenye whatsapp walipata wanakamati wote walikuwa ‘wameleft’ ! Walishangaa mbona walikuwa wameondoka kundi ambalo waliunda ili kuwasaidia kuchanga pesa za harusi na wao ndio waliokuwa pia wasimamizi .Jitihada za kuwapigia simu hazikufua dafu kwani simu zao zilikuwa zimezimwa .

Siku ya jumatatu tarehe 24 ,Peter na Jane waligundua ukweli kwamba wanakamati  wale walikuwa wametoroka na pesa zao na kugawana zile pesa .kwa sababu ya virusi vya Corona ,kila mmoja aliitumia hiyo kama sababu ya kwenda zake na wengine wameshaelekea mashambani . Harusi yao imekwama huku hela walizochangisha zikiibwa na watu waliowaamini na kuwapa jukumu la kuzichangisha na kuziweka .