Waluhya noma

Waluhya Waliwakosea nani? Vijembe 10 vya utani ambavyo vimetupatia Ucheshi

   Kenya  ,ni taifa zuri na lenye mvuto wa kipekee ambao hata wenyeji  ,wakati  mwingine tumejipata kuwa na fahari sana kuitwa wakenya .Jamii zetu mbali mbali pia zimechangia kuifanya nchi hii kuwa spesheli .Kutokana na maumbile  tofauti ,tabia  na mienendo mbali mbali ya jamii za Kenya ,mseto huu wa kila aina ya  jambo ndio unaotufanya kuwa Wakenya .Lakini endapo kuna jamii ambayo imefanyiwa soga sana mtandaoni  kwa njia nzuri na  ya utani ili kutuchekesha sote,basi  ni  jamii ya waluhya .  Aghalabu utani huu huhusisha mambo ya  mlo .  Baadhi ya vijembe hivi ni  vitu vya kila siku vyenye msingi wa dhana potovu ama kiasi Fulani cha ukweli  .Mengine yanatufanya tutafakari  uhalisia wa maishaya kijamii ya makabila yetu na mengine yanatufanya tuwaze hata zaidi .Mengi  hata hivyo   ni ya kweli na yanakwaza . Hii hapa orodha ya vijembe 10 vya utani kuwahusu waluhya ambavyo vimetupa tabasamu hata tunapokabiliwa na  nyakati ngumu .

 1.Kumeza sausage /smokie kama capsule

Now.Najua kuna  soga za kutuchekesha ,na tunaweza kujaribu kutafakari inavyowezekana ,lakini iwapo unajua capsule na jinsi dawa inavyomezwa –hebu fikiria kuchukua soseji    ikiwa nzima halafu uipurukushe  kinyuani.Matokeo  yatakuwa kitu kingine.utasakamwa lakini apparently jamii moja tu ndio iliyo na uwezo wa kufanya hilo .I surrender .

 2. Mluhya akila kuku ,anakula vyote, sauti na kivuli!

 Hii hata sitaeleza zaidi . Imetosha tayari jinsi ilivyo lakini nimechukua muda mrefu kufirikia jinsi unavyoweza kula sauti ya kuku  au hata unavyotayarisha kivuli cha kuku kuwa mlo .I give up .

Easy Come Easy Go: ‘Githeri man’ arejelea hali yake ya uchochole.

  3.Papa shirandula na Patanisho .

Hapa najua kuna tone  la ukweli .Nimeskia utani huu eti  ukitaka  msichana mluhya akupende kupindukia ,usiku mfungulie atazame papa shirandula  akinyofoa sima na kuku .Asubuhi mfungulie radio Jambo asikilize Patanisho ya Gidi na Ghost.Wiki moja baadaye panga harusi ! You are already romantic…. Kali sana .

 4 Gani tamu kati ya ugali na Keki ?

 Umesikia  utani huu wa  rafiki ambao wapo njia panda kuhusu zawadi ya kumpa rafiki yao mluhya.wakisema eti keki haitamridhisha na badale yake sima ndio zawadi tosha .Mluhya hujamridhisha  endapo hajakula sima . Inasemekana ni dharua kubwa sana kumpa  mwanamme mluhya wali kama chakula,hiyoni snack ama kiamsha   hamu tu. Vitu kama  spaghetti  ni mzaha sana kwa mluhya !

 5.Dem yako hushiba ama ni mluhya?

Hii  imekuwa ikibadilishwa kila uchao ili kutoa taswira mbali za kuvunja mbavu.Sijui ni  mtani yupi huyu aliamua kuja  nah ii  lakini najua umezisikia au kuzisoma .Mengine ya  kuchekesha ni maswali kama-Chali yako hukupea pesa za salon ama ni mluhya ? Boyfriend yako ni babyface ama ni mluhya?

 6.Unga,Posho mill na Sima

 Hizi najua wengi mmeziona kuanzia jadi . Nimeona tangazo  bandia la nyumba ya kukodi ambalo limeongezwa chumvi ili kusoma hivi –    A spacious Bedsitter,inbult wardrobes and a poshomill nearby.Ideal for luhyas!  Jamani najua waluhya wanapensa ugali ,lakini  hebu fikiria kuhusu mtu ambaye anaweza kuchagua nyumba ya kuishi kwa msingi wa owepo ya mashine ya kusaga mahndi au nafaka . Kisha kuna hii moja yenye picha ya bundi aliyefurahi na maandishi – kale kafeeling ka mluhya akisikia patanisho alafu advert ya Unga iwe next’.

 Wengine wameizidisha na kuweka utani kama ; Breaking News,Man dies after attempting to speak luhya language with an empty stomach . Halafu kuna hii nyingine – Ukipika ugali kubwa na mayai mawili ,inafika point unachuna ugali na unapoint mayai …

  Siwezi kusahau  picha za utani zilizoonyesha mtu aliyedaiwa kuwa mluhya ambaye alikuwa amezirai ,lakini pindi tu alipowekewa sima karibu na pua ,aliamka papo hapo !

Must Read: Still Single?Sababu 8 zinazokufanya usiwe na Mpenzi

 

 7.Chai .

 Hii ni  ya tangu jadi . umeskia mtu akinywa chai anaulizwa  – kwani wewe ni mluhya? Cha kuchekesha ni kwamba  najua watu wengi hata wasio waluhya wanaopenda chai .Sijui aliyeitunga hii alifanya utafiti gani lakini imetamba sana . Kisha kuna ule utani wa  mluhya aliyeanza kuchemsha maji ya kuoga lakini kati kati akabadilisha mawazo na kuweka majani ili iwe chai .

  Pia kuna  nyingine ya mluhya kulamba  sukari na kunusa  kahawa ndio apate feeling ya ‘breakfast’.

 

  1. Mazgwembwe

  Hii najua  mumeshaisikia na kuhusu  miguu ya waluhya iliyojaa,sehemu ijulikanayo kama ‘mazgwembe’ . nikapata kuiona moja kwenye twitter mtu akiuliza  – Kwa nini waluhya  hawananga pole dancers?

Mtu akajibu –

Hizo mazgwembe zao zitaangusha pole .

Hilo limeashiria maumbile ya kipekee ya waluhya walio na miguu minene na yenye nguvu .Najua waluhya ambao huitwa jina la utani ‘Stunya’.

 

  1. Matamshi ya B na P na D na T

  Kila jamii  ina athari Fulani ya kimatamshi  kwa sababu  ya muingilio  wa  lugha ya mama .waluhya hawajasazwa hapa na umesikia aghalabu watu wakiwaambia waluhya kuhusu kinachoonekana kama visawe katika matamshi yao.

 Sio purupuru ni buru buru

 Sio  matako ni ‘madhako’

 Sio Tisco ni Disco

 Kisha hii –

Saa hii Kuna mluhya anajua  ati Pope Collymore,Pope Marley na Pope Francis ni mabro . Ukatili!

  

10.Shortest Prayer

  Mengi yamesemwa ,na mengine zaidi kuandikwakuhusu wahubiri waluhya na  jinsi walivyo na passion katika kazi yao ya mahubiri . Imedaiwa kwamba wengi wa wahubiri hawa huomba kwa muda mrefu hadi kuwachosha waumini .Lakini  siwezi kusahau soga moja iliyozuka kuhusu jinsi ya kumfanya mhubiri wa kiluhya kufupisha maombi wakati wa hafla .Siri imesemwa aktika utani huo ni  kuhakikisha kwamba baada ya chakula kuwekwa mezani,hakikisha kwamba bakuli iliyojaa monofu ya kuku inaweza mbali sana na mhubiri . kwa sababu ya pupa ,atafupisha maombi yake  ili kuharakisha na kukimbilia ile bakuli na kuivuta upande wake! Huu ni ukatili .

 Tuambie ,ni vijembe vipi vya kuvunja mbavu ambavyo umeviona au kusoma mtandaoni ?

Photo Credits: radio Jambo

Read More:

Comments

comments