Wanafunzi 15 waliorejea nchini kutoka Sudan wapatikana na Covid 19

Wanafunzi 15  walowasili maajuzi Mombasa kutoka Sudan wamepatikana na virusi vya corona .

Waziri wa afya wa kaunti ya Mombasa  Khadija Shikely amesema wanafunzi hao walikuwa katika kundi la wanafunzi 129 waliosafirishwa kutoka sudan wikendi iliyopita . Walitua katika uwanja wa ndege wa JKIA Jumamosi wiki jana  baada ya kusafiri kutumia ndge ya KQ

Walifanyiwa ukaguzi wa matibabu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege  kabla ya kupelekwa katika  shule ya  serikali  ya  Kizingarea   ili kuwekwa karantini kwa siku 14.