Wafahamu? Wanahabari waliobarikiwa sura na sauti

Wanahabari huwa katika mstari wa mbele endapo watakosa ama watapatikana katika shida yeyote, lakini pia  sura na sauti zao huvutia hung'ata masikio ya wengi.

Hawa hapa  ni baadhi ya wanahabari wa Kenya ambao sauti zao hupamba masikio ya wengi kwa unga'to wa kusoma taarifa .

Jeff Koinange

Wow!! Tupilia mbali wazo la sura yake ngumu , sauti yake huvutia wengi pamoja na mahojiano yake, Jeff anafanya kazi katika runinga ya Citizen katika kipindi cha JKL.

Betty Kyalo

Katika mitandao ya kijamii anafahamika sana, si hayo tu uwaacha wengi wakimwaga mate kwa urembo wake na hata vile anavyo valia mavazi yake.

Tina Mwambonu.

Kichuna mrembo ,anayetoa wengi mate kwa sauti yake tajiki inayokupambia anga katika steshezini za Radio Africa ikiwemo Radio Jambo.

Tina sauti yake na macho yake ya kuvutia huwacha akina yahe wakimmezea mate kutokana na vile anavyosoma taarifa na hata anavyozungumza.

Dennis Okari

Mbali na familia yake Okari akisoma habari utapendezwa na sauti yake,amebarikiwa na sura ambayo wanawake wengi wangependa waume wao wawe nayo.

Doreen Gatwiri

Mmmh huwa tayari kuwashangaza mashabiki wake si kwa habari tu mbali kwa sura yake na pia mavazi yake, anafanya katika televesheni ya  NTV.

Lilian Muli

Kwa hakika hawezi saulika katikauwanja huu kwa sababu ya sura yake na pia kazi yake njema.

Swaleh Salim

Wakati wake wa kwanza kujulikana wengi walishindwa huyu mfalme wa sura nzuri ametoka wapi, na kwa kweli alibarikiwa na sura na hata kuwa na ujuzi wa kuwafurahisha mashabiki wake kwa mavazi yake yasiyo na wengi.

Lulu Hassan

Urembo wa kupigiwa mfano anao, mavazi si ya kawaida mbali ni ya kipekee, kwa hakika Rashid aliangukia kupata kipenzi kama Lulu.

Victoria Rubadiri

Si mwili mzuri si sura si urembo yote amebarikiwa nayo.