'Wanajinunulia maua na kusema ni wapenzi wao,'Huddah Monroe

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewashauri wanawake wajipende jinsi walivyo na vyovyote walivyo navyo na wala si kununua bidhaa kama maua na kuwasifu wanaume wao.
"Kama umakini kwanini umpe sifa mwanamme? naona wengi wakijinunulia maua na kuwasifu wanaume wao ilhali hawajazinunua jivunie chochote unachopata au mshahara wako." Aliandika Huddah.

Wengi walisema kuwa alikuwa anazungumzia aliyekuwa mpenziye Diamond Zari aliyekuwa anaposti zawadi zake kwenye mitandao ya kijamii na kumsifu mumewee.

Katika posti nyingine Huddah alikuwa na haya ya kusema,

"Hamna tatizo lolote kwa kujitegemea, hauhitaji kuhisi unapendwa mwanamme anahitaji kuwa bonus."