Ojaamong

Baadhi ya wananchi Busia wamtaka gavana Ojaamong kujiondoa afisini

Siku chache tu baada ya gavana wa kaunti ya busia sospeter ojaamong kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufujaji wa fedha za umma, baadhi ya wananchi wamejitokeza na kumtaka aondoke afisni kwa muda hadi kesi hiyo ikamilike wakidai kuwa ameanza kuwatishia mashahidi.

Kupitia kwa fugufugu la Busia Residents Association, wananchi hao wakiongozwa na Patrick Gomba Sewe, Concepta Omondi na Ali Mohammed wamemusuta gavana huyo kwa madai ya kuwahamisha wafanyikazi wa serikali yake wanaokisiwa kuwa mashahidi wakubwa kwenye kesi ya ufisadi dhidi yake.

Leornard Acharry Odhiambo

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments