Wanasiasa wa mlima Kenya wanaogopa kumwambia Ruto ukweli-Mwangi Kiunjuri adai

Aliyekuwa waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri amewaonya wanasiasa dhidi ya kumtegemea naibu rais William Ruto kufadhili kampeni zao za kisiasa.

Huku akizungumzia kumuunga mkobo Ruto alisema kuwa atamuunga mkono uaniaji kiti cha urais lakini akiwa kwa chaa chake.

Pia alisema ya kwamba Ruto amepewa mamlaka ya kumteuwa mwaniaji mwenzake, lakini kuna hofu ya kuwa na mamlaka mdogo kwenye serikali.

Kiunjuri alisema kuwa ni yeye pekee ambaye yuko upande wa Ruto na ambaye anamwambia ukweli kuwa ameangusha wakazi wa mlima kenya huku akidai kuwa wanasaisa wa upande huo wanahofu ya kumwambia ukweli.

"Tulizungumza na Ruto na tukakubaliana kuwa atamchagua mwenzake wa uwaniaji kiti cha urais kutoka mlima kenya, na mabaye anafahamika sana awe mimi,Ichungwa au Moses Kuria ama mtu mwingine yeyote nitamuunga mkono

Mpaka wakati huo uje nataka kujenga chama cha TSP kwa maana kupitia chama hicho nitampa naibu rais changamoto ya kuangalia watu wa mlima kenya 

Nikikuwa naibu wake nitakuwa na kifaa cha kuoigana vita kama mnavyoona kutokana na serikali hii mambo yanaweza enda mrama

kama katika mchakato wa ugavi wa mapato, mnaona wanasiasa au viongozi wa mlima kenya wanaogopa kumwambia naibu rais ukweli kuwa ameangusha watu wa mlima kenya."Kiunjuri Aliongea.

Alisema pia chama chake kimefungua ofisi 27 juu ya 27,huku akisema kuwa anaendelea kujenga chhama chake tangu afutwe kazi Januari.