NA NICKSON TOSI
Mtangazaji Kambua amefunguka na kusema amekuwa akivumilia kuelezea historia yake kwa umma jinsi alivyopata ujauzito kwa sababu wanawake wamekuwa wakimuuliza ni nini alichokifanya ndiposa akawa mjamzito.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na jarida la Parents Magazine, Kambua alisema hana majibu yoyote kuhusiana na maswali hayo .
Mama Nate kama anavyojulikana na watu wa karibu, alisema kuwa mwanawe Nathaniel ni miujiza kutoka kwa mwenyezi baada ya kubaguliwa kwa muda na jamii.
Aliongeza kwa kusema kuwa safari yake imekuwa ya manufaa zaidi katika mamia ya watu na kwa jamii kwa ujumla.
“I’m unafraid of having this kind of conversations because I know how it feels. My journey was painful, but it helped me speak up for other people who are constantly facing pressure from all kinds of places,” alisema Kambua.