EQpwwnaWsAsoCfR

Tena!!;Wanaume ambao hawakubaliwi katika mkutano wa wanaume

Leo ikiwa ni siku ya wapendanao duniani wanaume wengi wamo tayari kuenda katika mkutano wa wanaume kwa maelezo jinsi ya kukaa na wanawake wao.

Baadhi ya wanaume hao ni kama,

Wanaume wasio na ndevu

Hawakukosea waliposema mwanaume ni ndevu, katika mkutano huo wa wanaume kama huna ndevu ama huna dalili ya ndevu zako kuota tafadhali kaa nyumbani hamna nafasi yako huko

Msaidie mke wako kulea watoto.

wanaume walio na vitambi

Huu ni mwaka mwingine, hakuna haja ya kushindana na wanaume waliojaaliwa lkitambi,, katika mkutano huo au kongamano hilo nafasi yako tayari ishaa chukuliwa na mwingine.

Wanaume wanapenda kusengenya

Nadhani masengenyo tuliwachia wanawake hasa wale hawana kazi ya kufanya, kama una huo mdomo tafadhali kaa nyumbani usiende katika mkutano huo.

Wanaume wanao wasifu wake zao katika mitandao ya kijamii

Kama ni mapenzi yanatoka rohoni na unapompenda mtu iwe siri si kusifu mwanamke wako kila mahali jiekee siri, ata wale wanawachumbia wake zao hadharani ata hampaswi kuangalia lango kuu la mkutano huo.

Wanaume ambao wanawatumia wapenzi wao nauli

Kwanini utumie mpenzi wako nauli, ukituma wanakula na kisha wanaanza kutoa vijisababu ambavyo haviuna mwelekeo.

Kama ushawahi tuma nauli nakusihi kwa heshima zote usiende mahali popote.

Wanaume wanaovaa suruali zimewakamata

Kwanini uvae nguo ambayo huna amani nayo kila wakati nikujiangalia kama uko sawa, sababu ya mungu kuwaumba hivo alikuwa na sababu yake.

Wanaume ambao wameeka vipuli kwenye masikio

Urembo wachia wanawake, kama Mola aliona akuumbe jinsi ulivyo bila ya kuweka madoido kwenye mwili wako,yote tisa kumi ni usijaribu kutoa mguu moja mguu mosi kuenda katika kongamano hilo.

 

 

Photo Credits: radio jambo

Read More: radio jambo

Comments

comments