Wanaume wanaodhulumiwa na wake zao wahofia kupiga ripoti - Njenga

wanaume
wanaume
Kundi kumoja humu nchini limewaomba wanaume kutoficha visa ambavyo wamedhulumiwa na wake zao.

Kundi hilo lijulikanalo kama 'Voice of Men and Children' siku ya Jumamosi lilitangaza kuwa kati ya wanaume 10 ambao hupigwa na kutendewa maovu na wapenzi wao, ni watatu tu huripoti matukio hayo.

Mwenyekiti James Njenga aliwashauri wanaume kujitokeza na kuongea kuhusu wanayopitia mikononi mwa wake zao kwa marafiki zao, mhubiri au pia mshauri wa ndoa.

“Our aim is to ensure couples live peaceful, reduce incidences where they take each other before the police or other offices, by attaining responsible and solution-oriented families” Alisema.

Akizungumzia katika afisi zao zilizoko Limuru, Njenga alisema kuwa masaibu mengi hujulikana pindi tu wanaume wanapo jitia kitanzi.

“Men suffer a lot but they hide those sufferings. This very bad and unfortunate” Alisema.

Kundi la Vomec lilisajiliwa kama NGO mapema mwezi huu wa Disemba ili kuwapa mawaidha wapendanao, ili kupunguza visa vya kupeana talaka, kutengana, dhulma za kimapenzi, mauaji au kujitia kitanzi.

“Some of these issues happen, one spouse and the couple’s children are left suffering psychologically as well as financially,” Njenga alisema.

Hata hivyo aliwasifu wanawake akisema kuwa huwa hawafichi masaibu yao.

“Women rush to police or children’s offices to seek solutions. At times men are charged before court of law” Alisema.