Bus accident on Mombasa Road

Wanaume waongoza kwa idadi ya vifo kupitia ajali za barabarani

Wanaume wanaongoza katika vifo kupitia ajali barabarani, hii ni kulingana na mamlaka ya usafiri wa kitaifa na usalama (NTSA).

Katika kipindi cha Januari 2018 hadi Septemba 16 mwaka huo huo, NTSA ilirekodi vifo vya wanaume 1,756 walioangamia katika ajali.

Ni wanawake 386 pekee ambao walifariki katika kipindi hicho.

Je atawahi? Kipchoge ateuliwa kwa tuzo la mwanariadha bora wa mwaka

Hii inaashiria kuwa asilimia 83.3 ya vifo hivyo ni vya wanaume huku asilimia 16.7 per ikiwa wanawake.

Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka mwaka wa 2019 katika kipindi hicho cha Januari hadi Septemba. Mamlaka hiyo ilirekodi vifo 2,066 vya wanaume huku 417 vikiwa vya wanawake.

Kulingana na data iliyokusanywa na mamlaka hiyo, kutoka Januari 1, hadi Septemba 25, 2018, jumla ya vifo 2,219 vilirekodiwa.

Katika kipindi hiki, abiria 7,300 waliumia. Mwaka wa 2019 katika kipindi hicho, Kenya ilipoteza watu 2,591 huku jumla watu 8,596 wakiumia.

Data hizo zinaonesha kuwa kutoka Januari hadi Oktoba 1, watu 2,640 waliangamia kupitia ajali, ambalo ni ongezeko kuu ikilinganishwa na vifo 2,278 mwaka wa 2018.

Gari za kibinafsi ndizo zilizochangia katika ajali nyingi zikiongoza kwa idadi ya gari 702, magari ya kibiashara yalifuata na magari 597, bodaboda 542 huku gari za abiria zikifunga na 411.

Martial anatarajiwa kucheza dhidi ya Liverpool baada ya kuregelea mazoezi

Wananchi wanaotembea kwa miguu wanaendelea kuongoza katika idadi ya waliofariki kupitia ajali huku 1,033 wakiangamia mwaka huu, wakifuatiwa na abiria 542, waendesha pikipiki 537, abiria wa pilisi wakiwa 254, madereva 253 na waendesha baiskeli 53.

Hii ni ongezeko ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo vifo vya wananchi wanaotembea kwa miguu vikiwa 882, abiria 521, waendesha pikipiki 422, abiria wa pilisi 186, madereva 233 waendesha baiskeli 42.

PATANISHO: ‘I am busy muache kunilazimisha kuzungumza!’ – Paul

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments