Wanaume watatu wauwawa na sehemu zao za mwili kung'olewa

Wanaume watatu wauliwa kwenye mtaa wa Bomet na mmoja wao kuumizwa vibaya. VIlevile, walipopatikana inasemekana kuwa, walipatikana bila sehemu nyingine za mwili.

Polisi na viongozi wamekuwa na hofu kwani wanakisia huenda ikawa kitendo hicho kimehusiana na uchawi.

Mwanaume mmoja aliuliwa alhamisi na mmoja wao akaumizwa sana usiku wa Alhamisi. Vilevile manusuru mmoja alirekodi ujumbe wa polisi alipokuwa kwenye kitanda cha hospitali.

Musa Omari, komanda wa Sub county ya Bomet alisema kuwa, hawezi kata kauli na kusimulia yaliyotendeka kwani lazima uchunguzi ufanywe zaidi ili aweze kuwa na uhakika wa kitendo kilichofanyika.

Walioshuhudia walisema kuwa, huenda ikawa mauaji haya yalifanywa na wachawi waliokuwa wanatafuta sehemu za mwili zitakazo tumika katika ushirikina.

Alhamisi usiku, mwili wa jamaa mmoja aitwaye Stepehen Okoth ulipatikana kama hauna macho wala sikio la kushoto

Jamaa huyu alikuwa amepasuliwa kwenye mapaja pia na watu kusema labda wachawi hawa walikuwa wanataka sehemu iliyo na damu nyingi na ndipo wakaamua kukata mapaja.

Mwili wake uliachwa nje ya mlango wake.

Vilevile, wanaume wawili ambao walikuwa majirani, walikuwa wanaelekea nyumbani kwao na kabla ya kungia ndani ya nyumba yao, wakauliwa  na miili yao kuwachwa nje ya nyumba yao. Licha ya hayo, wauwaji wa majamaa hawa walitoroka na sehemu za miili zao.

 Wakaaji wa mtaa huo wa Bomet wanaomba uchunguzi ufanywe haraka ili washukiwa washikwe ndiposa waweze kujua kuwa wana usalama kwani wanaona ni kama wauaji hawa wanalenga watu wa mtaa mmoja.
Jamaa ya mwanaume aliyelazwa  hospitalini wanasema kuwa mwenzao majeruhi anawajua wauaji hawa na hivyo basi, wanaomba apate nafuu ili aweze kusema majina ya washukiwa hao na kuiokoa jamii yote.

Polisi waliomba wanajamii wa mtaa huu kuripoti ujumbe wowote watakaopata kwenye kituo cha polisi  ili iwe rahisi kwao kumkamata au kuwakamata washukiwa.