Wanaume wenye wake wengi watoa siri ya kuwapenda wote kiwango sawa.

wake.wawili
wake.wawili

Kama kuna kizungumkuti ambacho wengi hawajaweza kutatua ni jinsi wanaume walio na zaidi ya mke mmoja huweza kuwatosheleza wote kimapenzi.

Na hapa hatuzungumzii tu kuwatosholeza kitandani bali, kuwapa mapenzi sawa, kuwalinda, kuwalisha na kuhakikisha kila mmoja ana furaha kwenye ndoa.

Jambo hili huwa ngumu zaidi kwani ni changamoto kwa wake wawili kuishi kwa amani na bila wivu kwa ndoa, kwa sababu kila mmoja huvuta penzi upande wake na kujipata katika mashindano ya kung'ang'ania mume.

Tulipochapisha hoja hii katika ukurasa wetu wa Facebook, kuna jamaa aliyejitokeza na kusema kuwa ana wake wawili na cha kushangaza ni kuwa anawapa wote mapenzi sawa.

Jamaa huyu kwa jina la Samuel Mogambi, pia alisema wawili hao wanapendana na wanaheshimiana na hilo humsaidia kupunguza mipango ya kando.

Alisema;

Samuel Mogambi: Ndio kuna uwezekano (wa kuwapenda bibi zaidi ya mmoja kwa usawa) na inategemea vile mume umejipanga, mimi niko na wawili na wanajuana wananipenda pia nawapenda sana nikiwa pale huyu anajua niko pale Hiyo inapunguza mpango wa kando vile naona hayo ni maoni yangu

Hata hivyo baadhi ya wanajambo walikuwa na maoni tofauti na hii ni baadhi ya waliyosema;

Mark Wanyama: Hiyo yawesekana, kila mtu hujipima ndipo huja na uwamsi wake. Kwangu hata wawe kumi naweza kabisa

Brian Isinalo: Yes Niko na watatu na am 28years and I love them all

Mugun:  kinachofanya mtu aoe bibi labda ni maadili mpovu ya bibi wa kwanza.kwa hivyo mapenzi ya mwanaume anaelekeza kwa bibi ya pili kusema ukweli japokuwa haonyeshi.

Ben Xonko: Uwezekano upo Massawe tena xana iwapo wale wake wawili watakubali kujiona sawa na waondoe kuoneana wivu, kupelelezana na kudakiana (yaani kuongea udaku) kwa yule mume

Barnabas: In the beginning..... God created male and female...... for this reason two shall become one flesh...... when they come together in marriage....... God's mathematics is one flesh not two or three........