‘ Wanavuruga ndoa za watu’ Huddah azungumza kuhusu kukamatwa kwa Edgar Obare

Mwanasosholaiti  Huddah Mnroe  yupo Dubai  na akiwa huko amezungumza kuhusu  kuhusu kukamatwa kwa mwanablogu Edgar Obare   ambaye amekuwa akifichua mahusiano ya wanasiasa na   mahusiano yao  ya kimapenzi.

Amesema kukamatwa kwa Obare ni ishara ya jinsi watu wanaoeneza uvumi wanafaa kuadhibiwa kwa kuvunja ndoa za watu  ilhali masuala ya kibinafasi ya watu yanafaa kusalia siri .

 Huddah alisema ;

 Watu kama hao wanafaa kukamatwa  ,kupigwa na mikono yao kuvunjwa! Ili wasiweze tena kuchapisha  tena chochote katika maisha yao

Kero lake hilo lilielekezwa dhidi ya Edgar Obare  akimuambia awafichue watu ambao humpa habari hizo za siri .

Huddah aliyafichua hayo wakati wa maswali na majibu  alipowauliza wanachokosa kumhusu

Huddah hajasazwa siku za hapoo nyuma na wanablogu  kuhusu kazi ambayo  yeye hufanya  na pia alieleza kwamba anachukia sana uvumi na masengenyo