codom

Wanawake wahasiriwa wa mafuriko, waomba kondomu zaidi kuwatimizia wanaume wanaomezea mate

Afisa wa afya katika kaunti ya Kilifi alilazimika kukatisha mkutano wa umma na kuendea kondomu ili kuwapa wanawake waliohama  makwao na kukita kambi katika eneo la Magarini kutokana na mafuriko.

Zaidi ya wanawake 2,000 katika lokesheni ya Garashi walilalamikia kuwa watazidiwa na hamu ya mapenzi kutoka wanaume wanaowamezea mate baada ya kukaa pamoja nao kwenye mahema.

David Kakake Ruto, Asimulia Jinsi Maisha Yalivyokuwa Magumu Wakiwa Wadogo

Aidha wanasema kwamba wamekaa kwa majuma kadhaa mbali na wanaume zao, huku wanaume walioko kwenye kambi wakiwamezea mate.

“Kwa kuwa tumekaa hapa kwa zaidi ya majuma mawili bila wanaume wetu walioko kwenye mashamba wakichunga mali huku wengine wakiwa mbali kazini, tuna hamu za kimapenzi na tunaweza tukahadaiwa na wanaume kufanya mapenzi nao, mmoja wao alisema.

Picha Ya Siku: Mti Wa Krisimasi JKIA, Economy Ni Mbaya Hivi?

Afisa wa umma anayeshughulikia afya Amos Nthenge alikuwa amezuru eneo hilo kuona jinsi hali ilivyo, lakini wanawake hao wakaahidi kumsikiza iwapo ombi malalamishi yao yangeshughulikiwa.

Amepata Mpenzi? Maribe Asherehekea Birthday Na Busu Moto! (Video)

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments