Miaka chacha baada ya kifo cha Juma, mjane Lydia Tabuke amejitokeza na kusema yeye na watoto wake wawili wametengwa kwenye orodha ya wanaonufaika na mali hiyo iliyokuwa ya mume wake.
Anasema ametengwa na Miriam Wairimu aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mali ya Juma mnamo 2017.
Jacob Juma alikuwa mfanyabiashara maarufu na pia mkosoaji mkubwa wa serikali.
Alimiminiwa risasi na kufariki mnamo Mei 5, 2016, jijini Nairobi, na kuzikwa Mei 14 katika eneo la Mungore, kaunti ya Bungoma.
Mizozo ya mali kati ya familia yake ni moja ya safu ya kesi zenye hali ya juu ambazo zimekuwa zikiangazwa na vyombo vya habari hivi karibuni, miongoni mwao ni familia ya Koinange, Karumes, Michuki na JM Kariuki.
Ndugu ya Juma Francis Shiundu aliarifu mahakamana na kuthibitisha kwamba Tabuke pia alikuwa mke wa Juma.
Kwa sasa mjane huyo anarai kwamba ili kuthibitisha kuwa anastahili kushirikishwa katika ugavi wa mali ya aliyekuwa mumewe ,Tabuke anataka mahakama iwafanyie wanawe vipimo vya DNA.
Kulingana naye anataka vipimo hivi vifanyike katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (Kemri) na sampuli ya chembechembe hizo muhimu za DNA zichukuliwe kutoka kwa mamake Juma, Irene Adhiambo Juma.
Mara tu matokeo hayo yatapoatoka, yeye anataka yapelekwe kortini na Kemri.
"Iwapo uchunguzi wa DNA utadhihirisha kuwa wanawe ni wa Juma Jacob, wanaosimamia mali hiyo wanapaswa kulazimishwa kuwagawia yeye pamoja na watoto hao wawili kama inavyopaswa kunufaika katika mali hiyo." hati yake ya kortini ilikuu hivyo.
Nduguye Juma Shiundu anadai alikuwepo wakati wa hafla ya harusi ya kitamaduni baina ya Juma na Tabuke, ambayo ilifanyika kwa mujibu wa mila ya kitamaduni ya Luhya nyumbani kwao katika kijiji cha Nabuto, eneo la Mungore, kaunti ya Bungoma 2005.
"Najua marehemu alikuwa na watoto wawili na Tabuke. Alikuwepo pia wakati wa mazishi ya kaka yangu, ambapo nilianzisha wanawake wote na watoto wa kaka yangu wa marehemu kwa jamii, wageni na kila mtu aliyekuwepo kwenye mazishi, ” taarifa ya Shiundu inasoma.