Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu ...
Suluhisheni utata wa pesa za kaunti-Ruto
Naibu wa rais William Ruto amezitaka bunge na wizara ya fedha kusluhisha kwaharaka utata kuhusu kiasi cha fedha zinazofaa kupewa serikali za kaunti . Ruto amesema masuala yanayozuia kutolewa kwa fedha hizo yanafaa kujadiliwa na uamuzi kutolewa haraka ili kuepuka kuathiriwa huduma kwa wananchi katika kaunti .
IEBC yazuiwa kumwajiri afisa mkuu mpya
Mahakama ya leba imezidisha muda wa agizo la kuzuia kuajiriwa kwa afisa mkuu mpya wa tume ya IEBC .mahojiano ya waliituma maombi ya kazi hiyo yalifaa kuanza leo hadi jumatano lakini hilo sasa halitafanyika .jaji Byram Ongaya alitoa uamuzi huo katika kesi iliyowasilishwa na chama cha mawakili dhidi ya IEBC ,mwenyekiti wa tume hiyo na mkuu wa sheria .
Mfungwa aliyefariki katika gereza la Naivasha alipigwa
Matokeo ya uchunguzi wa mwili wa mfungwa aliyefariki katika gereza na naivasha wiki jana yameonyesha kwamba alifariki kwa ajili ya majeaha alipata baada ya kupigwa na kifaa butu . Simon gitahi mwenye umri wa miaka 35 aliaga dunia katika seli aliokuw amewekwa pekee yake baada ya kudaiwa kushambuliwa na maafisa wa gereza hilo.
Ukaguzi wa Ebola waendelea Malaba na Busia
Ukaguzi wa ebola unazidi kufanywa katika maeneo ya mpakani ya busia na malaba ili kuhakikisha kwamba walio na daalili za ugonjwa huo kutoka uganada wanatengwa . Everline walela kutoka wizara ya afya amesema pia wameweka ishara katika maeneo ya umma ili kuhamisha umma kuhusu ugonjwa huo.
Walimu wakuu waonywa kuhusu kuchomwa kwa shule
Waziri wa elimu George Magoha ameonya kwamba hatua zitachukuliwa dhidi ya walimu wanaokosa kuwazuia wanafunzi kuziteketeza shule .alikuwa akizungumzia kisa kilichotokea katika shule ya Upili ya Uriri ambapo wanafunzia waliichoma shule yao baada ya kuzuiwa kuutzama mchuano wa AFCOn kati ya Kenya na Algeria .
Usirauke kupiga foleni kupewa paspoti
Huna haja ya kurauka kupanga foleni kuanzia saa tisa usiku katika jumba la nyayo ili kuibadilisha paspoti yako endapo huna mpango wa kusafiri hivi karibuni . idara ya uhamiaji imesema itaendelea kutoa paspoti za kisasa hata baada ya agosti kwani zoezi hilo ni la kuendelea .
Wasimamizi wa elimu watakiwa kufanya ukaguzi wa kila mara
Wasimamizi wa elimu katika kanda wameshtumiwa kwa kuzembea kufanya ukaguzi katika maeneo wanayosimamia .waziri wa elimu George Magoha amesema kuna haja ya kuzidisha doria hizo ili kuhakikisha kwamba hakuna nja za kufanya udanganyifu katika mtihani wa kitaifa na pia kuzuia visa vya shule kuchomwa .
West Pokot yaanza kampeini ya chano dhidi ya Menengitis
Kaunti ya Pokot magharibi imeanzisha kampeiniya chanjo dhidi ya Menengitis kwa watu walio na umri wa mwaka moja hadi 29 .gavana John lonyangapuo amesema kampeini hiyo inawalenga watoto na watu wazima laki tatu walio katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Madaktari Kisumu warejea kazini
Madaktari huko Kisumu wameufutilia mbali mgomo wao na kusaini mkataba wa kurejea kazini na serikali ya kaunti . mwenyekiti wa muungano wao katika eneo la Nyanza Kevin Osuri amrewaagiza madaktari kurejea kazini mara moja
Wahudumu wa afya Taita watishia kugoma
Wahudumu wa afya huko Taita taveta wametishia kufanya mgomo kwa ajili ya kuchelweshwa kwa mishahara yao . mwakilishi wa muungano wao Kelvin Odongo amesema wamekuwa wakihangaika kila mwezi kwa ajili ya kucheleweshwa kwa malipo yao.
Mtihani wa gredi ya tatu kuanza Septemba
Wanafunzi wa gredi ya tatu watafanya mtihani wa kitaifa kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 16 hadi 20 septemba . Afisa mkuu mtendaji wa baraza la kitaifa la mtihani Mercy Karogo amesema mtihani huo utawawzesha kufahamu changamoto katika mfumo wa elimu wa CBC .matokeo yatatolewa mwezi oktoba .