"I want my belt back!" Zarika adai

NA NICKSON TOSI

Huo ni ujumbe wa mwanabondia wa humu nchini Fatuma Zarika ambaye ni bingwa wa zamani wa taji la WBC akiwa anaendelea na mazoezi yake Dubai.

Zarika alimshinda mpinzani wake kutoka Mehiko ama Mexico Yamileth Mercado japo november 16 katika pigano lililofanyika Chihuahua Mexico, Mercado alitawazwa bingwa mpya baada ya kumcharaza Zarika.

Zarika, ambaye kwa sasa anaendelea na mazoezi yake Dubai, amesema  iwapo bingwa huyo wa WBC atampa nafasi nyingine ya kupigana naye katika raundi nyingine yupo tayari.

Wakuu wa WBC walimwarifu bingwa Mercado kupigana na Catherine Phiri kutoka Zambia chini ya siku 90.

Pigano  hilo lilikuwa linatarijiwa kufanyika Machi japo kutokana na janga la Corona ikabidi kusongeshwa.