Wanyama aorodhesha mafanikio yake baada ya kujiunga na Montreal

Nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama amejiunga na Montreal Impact ya Canada, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 atajiunga na aliyekuwa mshambulizi wa Arsenal Thiery Henry ambaye ndiye kocha wa klabu hio huku  kilichosalia tu ni cheti cha uhamisho na kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Wanyama alijiunga na Spurs mwaka wa 2016, kutoka Southampton, na pia alichezea Celtic na Beerschot. Amekuwa na jeraha la goti lililomweka nje kwa muda mrefu na aliambiwa hakua katika mipango ya kocha aliyeondoka Mauricio Pochettino, na pia hajacheza mechi yoyote chini ya mkufunzi mpya wa Spurs Jose Mourinho.

Kupitia mtandao wake wa Twitter na Instagram, Wanyama ambaye kwa sasa anaonekana kurudisha tabasamu usoni mwake aliwashukuru mashabiki wa Spurs, kwa kuwa maishani mwake.

Isitoshe aliorodhesha mafanikio ambayo pamoja na wachezaji wenzake walisherehekea ikiwemo kumaliza wa pili katika ligi kuu ya Uingereza pamoja na kufika katika fainali ya ligi ya mabingwa bara Ulaya ambapo walishindwa na Liverpool.

I want to thank  fans for all the support over these past years,we have shared great times together from finishing 2nd in EPL to reaching the champions league finals,I will always be grateful for having be able to play for 

Wanyama pia alichapisha ujumbe wa pili akisherehekea kujiunga na Montreal huku pia akizungumzia imani yake kwa kocha Thierry Henry na uongozi wa klabu hiyo.

The Lion is coming to @MLS ,I’m really happy to join an exciting club like @impactmontreal I believe the Saputo family , @ThierryHenry

and the management at @impactmontreal have a great plan in place and I hope I can make a great contribution to the success of this project .

https://twitter.com/VictorWanyama/status/1235060407057952768

Tunampa Wanyama kongole na kumtakia kila la heri nchini Canada.