Wanyama atarajiwa kuchukua uraia wa Uingereza hivi karibuni

Nahodha wa Harambee stars na Totenham Hotspurs ya Uingereza,Victor Mugubi Wanyama anatarajiwa kuchukua uraia wake wa Uingereza ndani ya wiki zijazo.

Wanyama amefuzu kuchukua uraia huo baada ya kuishi nchini Uingereza kwa muda wa Miaka Sita.

Kulingana na katiba ya Uingereza, iwapo mja yeyote ataishi nchini humo kwa muda wa zaidi ya miaka sita basi huwa amefuzu kupata uraia wa nchi hio.

Hatahivyo,Wanyama anatarajiwa kuondoka ugani White Hart Lane msimu huu wa kipindi cha uhamishio wa wachezaji kufuatia ujio wa Tanguy Ndombele kutoka Lyon ya Ufaransa.

Msimu uliopita,Wanyama alikubwa na majeraha chungu nzima huku magoti yake yakiadhirija zaidi. Licha ya hayo, Wanyama aliweza kumaliza mechi za mwisho wa msimu akiwa fiti hata kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya AFCON kule nchini Misri huku akicheza mechi zote za Harambee stars.

Klabu yake Totenham Hotspurs ipo tayari kupokea dau lolote kwa uhamisho wa kiungo huyu mkabaji. Wachezaji wengine wanaotarajiwa kuigura Spurs wakati huu wa dirisha la uhamisho ni pamoja na mlinzi wa Ivory Coast Serge Aurier, Mshambulizi wa Uholanzi Vincent Janssen, Muingereza Kieran Trippier pamoja na Danny Rose.

Huku dirisha la uhamisho la nchini Uingereza likifungwa mapema kuliko Ulaya kote, Wanyama huenda akajiunga na klabu nyingine ya taifa lingine iwapo hatajiunga na klabu ya Uingereza wakati huu.

Kwingineko ni kuwa Eric Dier anatarajiwa kukosa mechi za  mwanzo wa msimu ujao kwani atakua anaendelea na matibabu yake ya kiuno aliyopata msimu uliopita.