Wanyama na Mariga wazungumza kuhusu ndoa zao

Victor Wanyama na kakaye mkubwa MacDonald Mariga ni baadhi ya wakenya wanaotamaniwa sawa na mabinti humu nchini kutokana na pesa yakishua wanayoingiza maishani mwao.

Wakizungumza kwenye kipindi cha runinga ya Citizen TV cha Jeff Koinange, madugu hawa wawili walizungumzia maisha yao ya ndoa jinsi wangependa kuishi ama kuoa. Jambo hili liliwavutia mabinti wanaowavizia kila uchao angalau wapate kujua ni lini watajipa raha nao.

Mariga alimjibu Jeff Koinange alipomuuliza kama atafunga pingu za maisha hivi karibuni kwa kusema kuwa anayapa maisha yake ya kisoka kipaumbele kabla ya ndoa maishani mwake.

Mariga kwa sasa anachezea klabu ya Real Oviedo nchini Uhispania.

" Nafikiri kuwa hilo ni swali ngumu ila kwangu mimi nimeipa taaluma yangu ya mpira itakua kwenye mstari wa mbele kabla ya ndoa yangu."

Nduguye mdogo Victor Wanyama aliongeza kuwa,

"Mimi sina shida ila nangoja wakati mwafaka ufike kisha kila kitu kitakuwa shwari."

Madugu hao wawili walienda kwenye shoo hio ndani ya gari lenye dhamani ya shillingi millioni 25. Kulingana na vyombo vya habari, madugu hawa wawili wanakisiwa kuwa na mshahara wa shillingi millioni kwa wiki.

Hatahivyo, wawili hao walikubali kuwa mshahara wao unatosha kuyakidhi mahitaji yoa na ya familia zao.

"Sijui pesa zenyewe ni ngapi kwani zinwekwa moja kwa moja ndani ya banki." Wanyama alisema.

Mariga anasema kuwa alitumia mshahara wake wa kwanza kumnunulia mamake nyumba moja ya kifahari kwani alikuwa anamsukuma sana amnunulie nyumba hata ingawa mshahara wake wa kwanza haukuwa wakupendeza sana.

Kulingana naye mariga, ilimbidi ajitolee kukosa vitu vingine ili aweze kumfurahisha mamaye mzazi.

"Nilipokuwa nasakata kambumbu kule uswidi, mshahara haukuwa mzuri sana ila mshahara wa kwanza nilimnunulia mama yangu nyumba kwani alikuwa anaitamani sana."Mariga alisema.

Mariga anajulikana kwa kuishi maisha ya kifahari pamoja na kupenda magari makubwa makubwa. Kwa upande wake wanyama, mshahara wake alitumia kununua shamba kisha akajenga nyumba yake.