Victor Wanyama ametemwa kutoka kikosi cha kwanza cha totnham Hotspurs cha mechi za kombe la mabingwa baada ya kocha Jose Mournho kukiri kwamba alikuwa na wachezaji wengi aliowazingatia mbele ya wanyama katika kikosi chake . Mourinho amesema uamuzi huo wa kumuacha nje Wanyama umetokana na ushindani mkali katika safi ya kati .Mechi za kombe hilo zitarejelewa tena mwezi huu .
Tottenham itachuana na RB Leipzig katika mkondo wa kwanza kwenye mashindano ya 16 bora februari tarehe 19 wakiwa nyumbani kabla ya mchuano wa mkondo wa pili mwezi ujao tarehe 10 baada ya kufika fainali mwaka uliopita .
Sheria za UEFA zinairuhusu timu kukifanyia mageuzi kikosi chake kabla ya awamu ya maondoano na Mourinho ameitumia fursa hiyo kumtema Wanyama ,nahodha wa kikosi cha Harambee Stars lakini akaamuakusalia na walinda lago watano katika kikosi cha wachezaji 30.