Wapendeza! Kutana na familia ya Dj wa nyimbo za injili, Dj Moz

Sanaa ya nyimbo za injili imekuwa na vuguvugu kwani wanamziki wengi, katika hii sekta wamekuwa wakifanya mambo pasi na wanavyo imba katika nyimbo zao.

Hata hivyo tunashukuru Jalali, kwani si wote wanaohusika na vurugu hizi kwani kuna wanamziki wengine wa injili kama Dj Moz ambaye yote anayo huburi kupitia kwa mziki wake unaambatana na anavyoishi maisha yake.

Moses Kimathi Mathenge, ajulikanaye kama Dj Moz ni Dj wa nyimbo za injili ambaye amekuwa kielelezo kwa jamii kwani jamaa huyu, ni baadhi ya wanamziki wa nyimbo za injili ambao wanaishi kulingana na maandiko.

Dj Moz alifunga pingu za maisha na mke wake kutoka nchi ya uingereza, Bi Deborah Kimathi, miaka chache iliyopita.

Harusi hii ilihudhuriwa na familia na marafiki wa karibu wa familia hii na mabingwa walio katika sanaa hii ya muziki za injili. Zaidi ya hayo, Dj Moz na Mke wake wamebarikiwa na watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume.

Vile vile, Dj Moz huwapa mashabiki wake, mawaidha kutoka kwenye Bibilia .

Baadhi ya mawaidha haya ni kama ifuatayo,

“AFTER WE HAVE WALKED AWAY FROM GOD AND FEEL LIKE WE HAVE WASTED OUR LIVES ON WORLDLY LIVING, MANY PEOPLE FEEL UNWORTHY AND UNLOVABLE TO COME BACK TO HIM. BUT HERE’S A GLIMPSE TO WHAT GOD DOES WHEN HE SEES US COMING BACK TO HIM: “SO HE GOT UP AND WENT TO HIS FATHER. “BUT WHILE HE WAS STILL A LONG WAY OFF, HIS FATHER SAW HIM AND WAS FILLED WITH COMPASSION FOR HIM; HE RAN TO HIS SON, THREW HIS ARMS AROUND HIM AND KISSED HIM. ‭‭LUKE‬ ‭15:20‬ ‭NIV‬‬.”

Hizi ndizo picha za watoto wake Dj Moz na mke wake,Deborah.