wafuasi

Wasanii 10 wenye ufuasi mkubwa nchini Kenya

Wasanii hujulikana umahiri wao kulingana na wafuasi alio nao kwenye mtandao wake wa kijamii hasa Instagramu na youtube. Kwenye orodha hii, tuangazie wasanii 10 wanao ongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wao wa instagramu.

Eric Omondi 2.4m

eric-omondi

Eric Omondi ni mvunja mbavu maarufu nchini Kenya. Omondi kwenye mtandao wake wa instagramu anawafuasi millioni mbili na hivyo kumfanya kuwa msanii anayefuatwa sana nchini Kenya.

Bahati 1.8 m

bahati

Baada ya kuanzisha show yake ya “Being Bahati,” mkali huyu wa nyimbo za injili alichukua nafasi ya pili kwenye orodha ya wasanii wenye ufuasi mkubwa kwenye mtandao wa instagramu kwani anawafuasi millioni moja na nusu. Bahati amekuwa akitamba na kibao chake cha mama.

Sauti Soul 1.5m

Wasanii hujulikana umahiri wao kulingana wafuasi alio nao kwenye mtandao wake wa kijamii hasa Instagramu na youtube. Wasanii hujulikana umahiri wao kulingana wafuasi alio nao kwenye mtandao wake wa kijamii hasa Instagramu na youtube.Sauti-Sol-e1437308272573

Kikundi hiki ndicho maaru zaidi nchini Kenya huku kikifuatwa na vijana wa Ethic. Sauti Sol inawakali wanne ambao ni; Bien, Polycarp Otieno, Chimano na Savara Mudigi.

Kikosi hiki kiliachilia Albamu yao ya kwanza mwaka wa 2005. Sauti Sol inawafuasi millioni moja na laki nne kwenye mandao wao wa instagramu.

Size 8 1.6m

SIZE-8-NEW-PICS

Size 8 kwa sasa ni mama na bibiye Dj Mo. Size 8 ana wafuasi millioni moja na laki sita kwenye mtandao wake wa instargamu. Mkali huyu wa ngoma za injili ametesa na kibao cha ‘Tamtam’ huku pia akitetemesha dunia kila wakati anapo achili kibao kipya.

Dj MO 1.3m

dj-mo-and-size-8..-e1518609102285-696x426

Sadfa iliyoje kupata bwanako anakufuata. Mkali huyu wa kutumbuiza kwenye maonyesho ya ngoma za injili anamfuata bibiye size 8 kwa kuwa na wafuasi wengi hapa nchini kenya. Dj Mo anawafuasi millioni moja na laki tatu kwenye mtandao wake wa instagramu.

Jaguar 1.1m

jaguar

Mbunge huyu wa Starehe aliwahi kutesa na kibao chake cha ‘One Centimeter Away’ kwa sasa anasherehekea kufikisha wafuasi millioni moja nukta moja kwenye mtandao wake wa instagramu. Jaguar amekuwa akifanya fani ya usanii pamoja na uanasiasa kwa pamoja.

Willy Paul 1.2M

willyp

Al maarufu kama pozze, Willy Paul anawafuasi milioni moja na laki mbili. Pozze amejizolea umaarufu wa kushangaza wengi hapa nchini akiwapiku wakali kama vile Khaligraph Jones.

Otile Brown 1M

otile

Aliyekuwa mpenziwe Vera Sidika anatesa na wafuaasi milioni moja. Otile Brown kwa sasa anatesa kibao cha ‘Baby Love’. Otile Brown anachukua nafasi ya nane kwa wakenya wenye ufuasi mkubwa nchini Kenya.

King Kaka 978 k

king-kaka5

Mkali huyu wa kidesign akishirikiana naye Eddie Butita anachukua nafasi ya tisa kwenye orodha ya wakenya wenye ufuasi wa mkubwa sana nchini kenya.

King Kaka ambaye kwa sasa amekuwa akitesa kwa wimbo wake ‘Wajinga sisi’ ameongeza wafuasi wengi na sasa ananusia wafuasi milioni moja.

Khaligraph Jones 966K

Khaligraph-Jones
Khaligraph-Jones

Khaligraph Jones ndiye rapa anayetabulika sana nchini kenya. Jones almaarufu kama papa anatesa kenya na dunia nzima na kibao chake cha Leave Me Alone. Jones anawafuasi laki tisa kwenye mtandao wake wa instagramu.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments