Njugush

‘Wasanii wanatamba sana mitandaoni” – Njugush

Mvunja mbavu Njuguna yuko tayari kufanya kazi na vijana. “Ethic, Ochungulo, Rico gang na Sailors ni wasaani wanaopendeza sana. Muziki wao una ujumbe ambao kila mtu anaweza elewa,” Njugush alisema akizungumza na Word IS.

“Mitandao ya kijamii imefanya kazi ya kufana sana kwani ingekuwa ni vyombo vya habari hawa vijana wote hawangefanikiwa walivyofanikiwa sasa.” Njugush alisisitiza.

Njugush ni mmoja wa wakenya wanotumia mitandao ya kijamii katika kufanya show zake.

“Mitandao ya kijamii inawapa watu steshoni na kutoka hapo vyombo vya habari vikuu vinachukua nyimbo zile na kisha kuzicheza.”

Njugush anawahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kutafta riziki yao.

“Haijalishi muziki wanaotoa, kusema ukweli ni kuwa tunao vijana wanaotumia vipaji vyao kujipatia riziki.”Alisema Njugush.

Njugush anasema kuwa serikali haifanyi vizuri katika kujenga nafasi za ajira na hiyo ndiyo sababu  vijana wanungana mikono na kufanya jambo litakalowasaidia.

“Naipenda lebo ya Odi pamoja na lebo zingine zote za vijana.” Njugush hivi majuzi alipewa tuzo la ‘Silver Play Button’ na mtandao wa Youtube. Tuzo hilo hupewa mtu anayefikisha wafuasi 100,000.

Tuzo nyingine za YOUTUBE ni : Gold and Diamond Creator Award, inayopewa mtu akifikisha wafuasi millioni moja na millioni 10. Njugush ako na wfuasi 180,000 kwenye  idhaa yake.

Hata hivyo,Njugush anasema kuwa lazima mtu aelewe hadhira yake ili aweze kuwapa ujumbe wanaohitaji. Pia anasema kuwa ile idhaa yako iwe na wafuasi wengi lazima uwape ujumbe kwa utaratibu.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments