'Wasanii wapaswa kujituma na kuwacha uvivu!' - Andrew Alovi

Andrew Alovi
Andrew Alovi
Andrew Alovi ambaye ni meneja wa mali ya masoko, Coke Studio alihudhuria studio za Radio Jambo ambapo pamoja na watangazaji Gidi na Ghost, waliangazia maswala ya wasanii wa kizazi kipya.

Huku mjadala wa kucheza mziki wa kikenya ukiendelea kunoga, Alovi ambaye ana talanta ya kugundua na kukuza talanta za wasanii humu na nje nchi, alikuwa na mawaidha kadha wa kadha kwa wasanii chipukizi.

Kulingana na Alovi, hata kama wasanii wanapigiania haki yao ya kupigwa jeki na watangazaji katika vyombo vya habari, basi wanapaswa pia wawache uvivu, wafanye utafiti vizuri na kisha wajue kujiuza kama wasanii.

Alovi alipeana mfano wa msanii Daddy Owen ambaye kwa ukakamavu wake alifanya utafiti na kutokea na nyimbo za 'Kapungala', mtindo wa kipekee na uliopendwa nchini na mataifa mengi.

Ningependa kuwahimiza wasanii tutie bidii, tufanye kazi. Hapo sasa tunaongelea wasanii ambao tunasema wana nyimbo nzuri, wana usanii na umaarufu." Alisema Alovi.

Aliongeza, Kuna wale wengine ambao hatutaki kuwa a bit strategic na muziki ambao tunafanya, utaingia studio uchukue mic kisha usema kile ambacho kitakuja kwa akili kisha useme mziki ndio huo. Nikikuuliza huo mziki wako unalenga nani, hujui. 

Hatuna mpangilio na mwelekeo, kuna kazi pale tuwache uvivu.

Chukua nafasi nenda usomee musicality ujue muziki unaenda namna gani na ni mitindo ipi ambayo inajitokeza."

Alovi alipeana mfano na msanii maarufu Diamond Platnumz ambaye licha ya kutambaa Afrika na duniani, bado hutia bidii na kujiuza katika nchi tofauti ili aweze kujijenga zaidi.

Tumchukue msanii kama Diamond, tunalalamika eti nyimbo zake zinachezwa sana Kenya. In the last 12 months Diamond amekuwa Kenya mara ngapi? Kuja kuuza mziki wake, kufanya concerts na kuongelesha makampuni kusema nina huu mradi ningependa tufanye.

Maanake licha ya umaarufu wake hakukaa Dar es Salaam, akasema liwe liwalo mziki utaenda vile utaenda. alitia bidii. Aliwashauri wasanii.

&feature=youtu.be