Wasanii waunguna kuchangisha fedha za mazishi ya Papa Dennis

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Papa Dennis aliyeaga dunia wikendi iliyopita atazikwa Jumatano wiki ijayo.

Gwiji huyo aliyejinyakulia zawadi tele, alipatikana ameaga dunia karibu na makao makuu ya chama cha Jubilee, pangani akikisiwa kuanguka kutoka orofa ya saba.

Mipango ya mazishi inaendelea huku kamati ikikutana Nairobi maeneo ya Biashara Street katika hoteli ya Country Cooking Hotel, karibu na Yala Towers. Kamati hiyo hukutana kila siku kuanzia mida ya saa kumi na mbili jioni hadi saa tatu ili kuchangisha fedha za mazishi.

Msanii Ringtone ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa studio za Nairobi Records Mash Mjukuu alisema kabla ya mazishi kutakuwa na misa ya wafu katika kanisa la Nairobi chapel, barabara ya Ngong jumatatu kuanzia saa saba hadi saa kumi.

"His body will later on that day be transferred to Matunda, Kakamega county. On Tuesday, there will be a public viewing of the body at his home in Matunda town. On Tuesday night, there will be another service conducted by Kenyan artistes," Mash alisema.

Wasanii wengi wamejitokeza na kusaidia mikakati ya mazishi yake.

"We need to put something together and support the family at this time and give Papa Dennis a decent send-off. Any amount is welcome," Mash alisema.

Kama unapanga kuchangia shughuli hiyo waweza tumia number ya paybill 7029669, jina ya akaunti ikiwa jina lako.