Wamesema Mudavadi hatofaulu katika azma yake ya kuwa rais endapo hatokoma kuwashambulia viongozi wa ngazi ya chini katika chama cha ANC walio na uwezo wa kumsaidia kuafikia ndoto yake yake ya kuwa rais .
Wakiongozwa na Livistone Omwakwe, wazee hao waliokuwa wakizungumza katika Central Villa Hotel Mjini Luanda siku ya ijumaa wamesema Mudavadi anahitaji msaada wa viongozi wote kutoka eneo hilo ili kuweza kuiga jeki jitihada zake za kuongoza nchi .
Hii ni baada ya habari kwamba chama cha ANC kimemfurusha seneta wa kakamega Cleopahs Malala kwa kukaidi msimamo wa chama wakati wa uchaguzi mdogo wa kibra mwaka jana ambapo alimuunga mkono mgombeaji wa ODM Imran Okoth badala ya mgombeaji wa ANC Eliud Owalo .
ANC pia kimefurusha mbunge mteule Geoffrey Osotsi. Chama hicho kimedai kwamba alitumia vibaya pesa za chama na kukiuka kanuni za ANC .
Lakini wazee hao wamepuuza madai hayo dhidi ya Osotsi, wakisema hangeweza kutoa pesa za chama bila idhini ya mwenyekiti au mweka hazina ambao sahihi zao zinahitajika .
Omwakwe amesema Mudavadi anafaa kufanya kazi na wanachama wote wa ANC na vongozi wao ili kukiboresha chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022 .